Kansela Rishi Sunak ambaye ni waziri wa fedha pamoja na waziri wa afya nchini humo Sajid Javid wamejiuzulu wakipishana dakika 10 tu wakati wakitangaza maamuzi yao, huku mawaziri wengine wadogo nao wakijuzulu.
Idadi inayozidi kuongezeka ya wabunge katika chama chake tawala cha Kihafidhina wanasema, wakati umewadia wa Johnson kujiuzulu.
Lakini Bwana Johnson ameonyesha azma yake ya kutaka kusalia madarakani kwa kumteua Nadhim Zahawi ambaye alikuwa waziri wa elimu, kama waziri mpya wa fedha mbali na kujaza nafasi zengine zilizokuwa zimeachwa wazi.
Baadae leo Johnson atafika mbele ya bunge kwa ajili ya kuulizwa maswali.