Jumatatu , 23rd Oct , 2017

Wanafunzi wanne wa shule ya sekondari Geita wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga mwenzao na kumtishia kumuua.

Wanafunzi wakiandamana (sio ya tukio husika)

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamisha Msaidizi wa Jeshi la Polisi Geita ACP Stanley Turiamo, amesema tukio hilo limetokea baada ya wanafunzi hao kumpiga mwanafunzi mwenzao wa kidato cha tano na kisha kumtishia kumuua, kitendo kilichopelekea kukamatwa kwao na kufikishwa mahakamani, kitendo kilichopelekea kuibuka kwa vurugu kubwa shuleni hapo.

ACP Turiamo ameendelea kusimulia kwamba licha ya vurugu hizo, wanafunzi pia waliwapiga kwa mawe bodi ya shule ambayo ilifika shuleni hapo kujadili suala lao, na kugomea kula kwa siku nzima.

Msikilize hapa chini akismulia tukio zima