Ijumaa , 26th Aug , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuchangia kwa moyo huduma za afya wanapoenda kupata matibabu katika hospitali za mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella

Akizungumza wakati wa kukabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo, Shigella amesema gari hilo limepatikana kutokana na michango ya wananchi hivyo waone kwamba kuchangia huduma ya afya kutasaidia kuimarisha sekta ya afya zaidi.

“ Wananchi wapennde kuchangia huduma za afya kwa moyo kwani kwa kufanya hivyo ndivyo tutazidi kuboresha huduma hizi na zikipatikana fedha nyingine tutaleta gari lingine ili kuweza kusaidia wananchi” Amesema Shigela

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Asha Mahita amesema , hospitali hiyo inakusanya milioni 70 mpaka 100 kwa mwezi ambapo kwa sasa bado mfumo wa kulipia huduma kwa njia ya kielektroniki haijaanza kutumika hivyo mfumo huo ukianza mapato yataongezeka zaidi.

Hospitali ya Bombo inahudumia wananchi kutoka wilaya 8 za mkoa wa Tanga na wengine kutika maeneo jirani.