Jumatano , 29th Mar , 2017

Chama cha Mapinduzi CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi an Uenezi wa chama hicho ndugu Humphrey Polepole, leo kimetangaza majina ya wagombea 12 watakaowania nafasi 6 za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Humphrey Polepole

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Polepole amesema kuwa Kamati Kuu ya chama hicho imezingatia Uadilifu, Uaminifu, Uzalendo, Uchapakazi, Maarifa ya mgombea na kuiishi Imani ya mwanachama wa CCM.

Kwa mujibu wa mchakato, wawakilishi kutoka CCM wanatakiwa kuwa 6 ambapo kati yao wanne watatoka Bara (wanawake wawili na wanaume wawili) na wawili watatoka Zanzibar (mwanamke mmoja na mwanaume mmoja) na kufanya uwakilishi uwe na uwiano wa 50% kwa 50% upande wa uwiano wa kijinsia.

Hawa ndiyo waliopitishwa kati ya wanachama 450 walioomba ridhaa hiyo.

Wanachana hawa 12 wataanza kampeni na kuomba kupigiwa kura na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloanza vikao vyake Jumanne wiki jayo.

Wabunge hao pia watakuwa na kazi ya kuchagua wajumbe watatu kutoka vyama vya upinzani.