Jumamosi , 24th Sep , 2016

Mashambulizi katika mji wa Allepo nchini Syria yamewaacha wakazi zaidi ya million moja bila huduma ya maji baada ya kuharibiwa kwa pampu ya maji Umoja wa Mataifa umesema.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto, UNICEF, limesema kuwa pampu ya kutoa maji ya Aleppo imeharibiwa. Wafanyakazi watano wa kutoa misaada wamejeruhiwa huku ndege za jeshi za Serikali zikiendelea kushambulia mji wa Aleppo.

Shirika hilo limesema mapigano hayo yamezuia juhudi zozote za kufanyia marekebisho pampu hiyo.

Taarifa zimeeleza kuwa watu 91 waliuawa katika mashambulizi ya Ijumaa na majengo 41 kuharibiwa.