Ijumaa , 24th Mar , 2017

Mkali wa hip hop kutoka 'Weusi', G Nako Warawara amekanusha zile tetesi zilizozagaa kuwa wimbo wake mpya ’Go Low’ aliofanya na Jux ni wa ku-copy na ku-paste kutoka kwa Flowking Stone wa nchini Ghana na kusema kuwa inawezekana idea zikawa zimefanana.

Jux na G nako wakiwa pamoja picha ambayo imetumika kwenye video ya 'Go Low'

Tuhuma hizo zimekuja pindi msanii huyo alipoiachia ngoma hiyo ndipo wadau na wapenzi wake kusema kazi hiyo imefanana  kuanzia jina mpaka ‘mixer’ za mdundo wa muziki huo ambao unafananishwa na 'Go Low' ya Flowking

“Mimi sijawahi kusikia hii nyimbo ‘before’ wala kumsikia huyu msanii ‘to be honestly’ na siku zote mimi siamini katika ku-copy kazi ya msanii mwingine kwa sababu naamini kabisa siwezi kupata njia yangu mimi kama ninaweza kumkopi msanii mwingine”. Alisema G Nako wakati akizungumza katika kipindi cha eNewz

Aidha msanii huyo amesema haiwezekani mtu akawa ana-copy na ku-paste halafu akapata njia yake anayoitaka kama utakuwa na 'vision' katika kazi zako na kitu chako.

Vile vile G Nako amesisitiza kuwa laiti angejua au kusikia wimbo huo upo katika mzunguko asingeweza kupoteza muda wake kutengeneza video na kurekodi sauti.

Kwa upande mwingine amesema 'idea' kama hizo za aina ya Club huwa zinatokea akiwa studio na siyo kwamba anakuwa amejipanga kuzipania kuzifanya.

Ngoma zenyewe hizi hapa, unaweza kuzitazama na ukatoa maoni yako.

Go Low ya Flowking
Go Low ya G Nako