Jumapili , 20th Sep , 2020

Msanii kutoka nchini Zimbabwe King 98 amefunguka kuhusu kufanya collabo na msanii na Boss wa Konde Gang mtu mzima Harmonize pia ametaja watu anaowapa nafasi kwenye maisha yake.

Kushoto ni msanii Harmonize, kulia King 98 kutoka Zimbabwe

Kupitia show Friday Night Live ya East Africa TV King 98 amesema hakuna kufanya kazi na Harmonize kwa sababu hata nchini kwao Zimbabwe wapenzi wa muziki wanamkubali sana.

"Kufanya collabo na Harmonize sio kitu kibaya, na kizuri zaidi ni msanii mkubwa  ambaye hata nchini kwetu watu wanamkubali hivyo ningependa nifanye nae kazi" amesema King 98 

Aidha akizungumzia kuhusu maisha yake binafsi nje ya muziki King 98 ameeleza kuwa "Vitu ninavyopata maishani mwangu ni baraka, siwezi kuwapa watu nafasi kwa ajili ya vitu vingine nafanya kazi ili watu waone, muda wangu mwingi natumia kwa ajili ya mama yangu, na  mpenzi wangu na mtu ambaye  ananishawishi ni baba yangu".

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.