Ijumaa , 20th Jan , 2017

Baada ya Rapa Young Killer, Roma na Nay wa Mitego kutaja list ya wasanii wa Hip hop ambao wanawakubali kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Rapa Nash MC amefunguka na kuwataja wasanii wa rap ambao anawakubali

Nash MC

Nash amekuwa tofauti na wengine kwa kutomtaja msanii hata mmoja wa hip hop na kusema kuwa aliyekuwa star wa twanga Pepeta, Ferguson ndiye mfalme wa marapa Tanzania.

Nash MC amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema kuwa anaomba orodha yake hiyo ya wasanii watano anaowakubali iheshimike.

Ferguson

 

"Naona siku hizi kila mmoja anataja Marapa wake bora anaowakubali. Sina budi na mimi niwatajie orodha ya wakali wangu hao watano. Nao ni
1. Khalid Chokoraa
2. Totoo Ze Bingwa
3. Msafiri Diouf
4. Canal Top 
5. Khalidjo Kitokororo Kuku

Ukitaka bonus nakutupia mzazi Ferguson mfalme wa marapa Tanzania naomba orodha yangu iheshiwe