Jumanne , 18th Jul , 2017

Msanii Nandy amedai kwa sasa yupo kwenye mazoezi makali ili kutengeneza mwili  mzuri wenye muonekano na mvuto mbele za watu.

Mwanamuziki wa kizazi kipya Nandy

Mbele kamera za eNewz ya EATV, Nandy amekiri hayo na kusema kuwa amekuwa akipokea ushauri kwa watu mbalimbali wakimtaka atengeneze muonekano na ndio ameanza mazoezi 'squat' kutengeneza tumbo pamoja na 'shape'.

"Nataka nitengeneze 'shape' yangu iwe nzuri, niwe na muonekano wa mazoezi. Na kwa vile mimi ni mtu wa kufanya show natakiwa niwe strong japo sina tumbo kubwa nataka niwe na six pack lakini 'very sexy'. Mimi nina ndoto za kuwa msanii wa kimataifa hivyo muonekano kwangu ni kitu cha muhimu isitokee siku nakutana na Ciara akaanza kunishangaa. Mfano aseme huyu katokea wapi", Nandy alisema.

Nandy ameendelea kufunguka "Sitegemei kufanya Surgery kujiongezea chochote kile, labda itokee siku moja nikanenepa kwa vile sasa hivi miili haikubali kwani tunatafuta maisha kwa nguvu zote. Ikitokea nimenenepa watu wasidhani nimefanya upasuaji kwani unene na surgery vinatofautiana lakini mazoezi nayofanya yatanitengenezea shape kidogo" aliongeza.