Alhamisi , 19th Jan , 2017

Rapa Nay wa Mitego baada ya kusikiliza wimbo wa Madee 'Hela' katika kipindi cha Planet Bongo EA Radio amefunguka na kumtaka msanii kutoka 'WCB Wasafi' Rayvanny kuja kumsaidia kaka yake huyo (Madee) katika uandishi.

Nay wa Mitego

Nay amesema kuwa akisiliza wimbo huo anaona kuna haja Raymond kumsaidia Madee kuandika kwani katika wimbo huo yeye amependa 'beat' kwa kuwa ni beat kali pamoja na baadhi ya vitu lakini kwenye uandishi wa wimbo huo 'Hela' hakuna kitu.

"Kwanza huu wimbo ni wimbo wa nani? Madee huyu huyu naye mjua mimi? Hii mistari napoisikia naona kuna haja Raymond aje kumsaidia kaka yake kuandika mistari. Aisee Raymond huyu Madee ni baba yako, huyu ni kaka yako njoo umsaidie, nasikiliza huu wimbo nakuona Raymond unahitajika kuja kuwasaidia kaka zako ambazo walikusaidia mpaka leo umefikia hapo" alisema Nay wa Mitego 

Uamuzi huu wa Nay kuiponda waziwazi kazi ya Madee unaweza kuzaa vita mpya ya maneno au ya kazi kati ya wasanii hawa wawili ambao wote wanatokea Manzese

Madee