Nikki adai Zilla ana-Stress

Saturday , 17th Jun , 2017

Rapa Nikki Mbishi amedai Godzillah anaumizwa na 'stress' za kuporomoka kimuziki kitu ambacho hakukitarajia kutokea mapema kwenye maisha yake ndio maana amekuwa akitapa tapa kwa kumtolea maneno ya kashfa kwenye kila mahojiano anayofanya.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo, Nikki amefunguka na kusema kwamba Mfalme huyo wa Salasala alibebwa na watu kwenye muziki na ndiyo waliomtupa na sehemu ambayo imemfanya ashindwe kuamka sababu inayomfanya hata kufikia kumtaja kwenye mahojiano mara kwa mara ili azidi kusikika.

"Zizi ameshushwa na waliompandisha bila yeye kutarajia hilo. Ametupwa halafu ameenda kuporomokea sehemu ambayo hata hajui atanyanyukaje, halafu ana watu wake anahitaji kuwasema ila anaona Nikki mwanangu nikiongea nitammudu fresh, kwanini awe muoga mbona mimi nawaambiaga,” Nikki alifunguka.

Aidha Nikki amejibu kauli ya Zillah kumuita 'Wack' na kusema kuwa haelewi ni sababu gani zimemfanya msanii huyo kutumia kauli hiyo huku akihoji labda kama anaishi maisha ya kuigiza kama msanii huyo ingekuwa sawa..

'Ukiniita mimi 'wack' kwa maana ipi, labda sijui kuandika, au 'wack' kama yeye hajui anachokifanya? anaishi maisha ya kuigiza, kujifanya wewe unaisha maisha ya Ulaya wakati upo Salasala unadanganya watu kuna all stars zimeninginizwa kwenye nyaya za umeme whichi is not true. Ana stress zake kaenda kwenye ufalme ambao sio wake sasa karudi huku ambako pengine alitakiwa awepo amekuta wafalme ni wengine na sio yeye tena,” Nikki aliongeza.

Recent Posts

Simon Msuva na Haruna Niyonzima

Sport
Msuva amlilia Niyonzima

Makamu wa Rais Samia Suluhu

Current Affairs
Serikali yetu haitarudi nyuma - Samia

Rais Magufuli.

Current Affairs
Rais Magufuli awachimba biti wanafunzi

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa

Sport
Mkwasa kuwashika koo waliochoma jezi

Msanii Dogo Janja Kushoto, na Kulia ni Mfanyabiashara Muna Love

Entertainment
Dogo Janja aruka kwa Muna Love