Ijumaa , 27th Nov , 2020

Mkali wa muziki wa dansi hapa nchini Tanzania Ali Choki amefunguka kusema ana jumla ya watoto 9 na wajukuu watatu, na watoto hao amewapata kwa mama tofauti wakati anahangaika kutafuta.

Msanii wa dansi Ali Choki

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Ali Choki amesema kwenye kipindi cha ujana wake alikuwa anaishi sehemu nyingi lakini sasa hivi ameshakuwa mtu mzima hivyo ametulia na kulea watoto wake.

"Kusema ukweli mimi nina watoto wengi jumla yake wapo 9 na wajukuu watatu, kwenye kutafufuta unaweza kuwa na mama tofauti lakini cha umuhimu watoto wako unawajua, kwa kipindi cha ujana nilikuwa naishi sehemu nyingi lakini sasa hivi tumeshakuwa watu wazima, unaamua kutulia na kulea watoto wako" amesema Ali Choki 

Aidha Ali Choki ameongeza kusema anajivunia kuwaona watoto wake kwa pamoja pia wanaridhika na kile kidogo ambacho wanakipata.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.