Jumatatu , 22nd Mei , 2017

Rapa Stamina amefunguka na kusema yeye hawezi kubishana na serikali na wala hakuna mtu anaweza kufanya hivyo  kwa kuwa nguvu ya mtu mmoja mmoja haiwezi kushinda nguvu ya serikali.

Stamina alisema haya alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live, na kusema amesikia kauli ya Waziri Mwakyembe inayowataka wasanii kuacha kuimba kuhusu siasa na kusema itabidi waifuate tu ingawa anaona ni kama wananyimwa haki yao ya kufanya kazi ya sanaa.

"Kama ulivyosikia kauli ya Mh. Mwakyembe kwamba  wasanii  tusiongelee masuala ya siasa, unajua huwezi kushindana na serikali yaani hiyo ni nchi nzima iko hivyo kwamba nguvu yako wewe binafsi haiwezi kuizidi nguvu ya serikali kwa hiyo muda mwingine tunafuata matakwa ya kile wanachokisema lakini harakati bado ipo pale, muziki wa Hip hop unahusu maarifa, ujumbe, content za kitu unachoongea kwa hiyo mimi nadhani kuna kitu kimoja hakipo sawa maana kama tunanyima uhuru wa sanaaa kiasi fulani"- alisema Stamina