Jumamosi , 22nd Nov , 2014

Zoezi la kuwasaka wanamitindo wenye muonekano makini kwa ajili ya kutokelezea kuonyesha mitindo ya mavazi katika jukwaa la Swahili Fashion Week kwa mwaka huu, limefanyika leo kwa mafanikio makubwa jijini Dar es Salaam.

Majaji wakiwa makini taytari kwa kuchagua Wanamitindo watakaoshiriki Swahili Fashion Week 2014.

Mchongo mzima umefanyika Msasani katika hoteli ya Sea Cliff ambapo wanamitindo wengi wamejitokeza kwaajili ya kuwania nafasi hii kubwa.

Vigezo ambavyo vimekuwa vikitazamwa kwa wanamitindo hawa ni urefu usiopungua sentimita 172 bila viatu virefu kwa wanawake na, sentimita zisizopungua 180 kwa mwanaume + muonekano wa kuvutia.

Usikose kutazama eNewz kesho, na kufuatilia Nirvana kuanzia wiki ijayo kujionea kilichojiri katika zoezi hili kwa ukamilifu.