Jumapili , 28th Aug , 2016

Msanii Niki wa Pili ameitaka jamii kuhamasisha watoto kupenda kusoma, na sio kuwafundisha kujua kusome pekee.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kuona habari iliyoandikwa na www.eatv.tv iliyosema "Wanafunzi 10,273 shule za msingi hawajui kusoma", Niki wa Pili aliandika ujumbe ambao ulionekana kugusa mashabiki zake huku wakimuunga mkono, ulioitaka jamii kuhamasisha watoto kupenda kujua kusoma.

"Kabla ya kumfundisha mtoto kusoma....kwanza mfundishe utamu wa kujuwa kusoma, raha ya kujuwa kusoma, uzuri wa kujuwa kusoma, kifupi usimfundishe kusoma, mtamanishe kujuwa kusoma, mfanye iwe ndoto yake, then the rest will be history, lets not teach, lets inspire the kids to learn", aliandika Niki wa Pili.

Niki wa pili ambaye pia ni msomi mwenye PhD yake mfukoni, aliendelea kwa kusimulia kile kilichomsukuma yeye kupenda kusoma na pengine ndio sababu ya kumfikisha hapo alipo, na kutueleza kuwa kaka yake ambaye pia ni msanii mwenzake Joh Makini, ndiye aliyemshika mkono na kumuonyesha njia sahihi.

"Nakumbuka Joh Makini ndio mtu alinifundisha kusoma na kuandika hata kabla sijaanza shule, kifupi alinifanya nika fall inlove na kusoma na kuandika, since msukumo ulitoka ndani ilinichukuwa muda mfupi sana", aliandika Niki wa pili kwenye ukurasa wake wa instagram.

Kwa upande wa mashabiki wake walimpongeza kwa ujumbe huo wenye kuigusa jamii, huku baadhi yao wakiandika haya..
Masanjalino: Una akili nyingi sana we braza nitamwambia magufuli akutumie.
scottermike: We jamaa unaakili sana,much respect

Post aliyoandika Niki wa pili kuhusu kuhamasisha kusoma