Ijumaa , 27th Mei , 2022

East Africa TV na East Africa Radio kwa pamoja leo walizindua Kampeni ya Namthamini 2022 katika shule ya Sekondari Kidete, Wilaya ya Kigamboni kwa mwaka wa sita.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidete na Kibugumo.

Kampeni hii ilianzishwa mwaka 2017, kwa lengo la kuchangisha taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji mashuleni.

Kwa mwaka 2022 imeanzia katika wilaya ya Kigamboni katika shule ya sekondari Kidete, na ilihusisha shule mbili za sekondari, wenyeji Kidete na sekondari ya Kibugumo.

Jumla ya wanafunzi wa kike 805 watanufaika na taulo za kike kwa shule zote mbili, ambapo Kidete ina jumla ya wanafunzi 407 wa kike na Kibugumo ina jumla ya wanafunzi 398 wa kike.

Jumla ya Pakiti 3572 za taulo za kike ziligawanywa kwa shule hizo mbili, kila shule imepata pakiti 1786.