Ijumaa , 13th Oct , 2017

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema mshambuliaji Sergio Kun Aguero anaweza kurejea uwanjani kesho kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Stock City.

Mshambuliaji huyo ambaye ameanza msimu huu vizuri alivunjika mbavu kwenye ajali ya gari jijini Amsterdam Uholanzi wiki mbili zilizopita.

Akiongea leo kwenye mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo wa kesho Guardiola amesema nyota huyo anaendelea vizuri na kesho ataamua kama acheze au aendelee kupumzika.

“Kuhusu Aguero yupo vizuri kuweza kucheza ila kesho ndo nitajua kama nitamchezesha au ataendelea kupumzika”, amesema Pep Guardiola.

Manchester City ambayo inaongoza msimamo wa EPL ikiwa na alama 19, kesho itakuwa nyumbani Etihad kuikaribisha Stock City yenye alama 8 katika nafasi ya 13.