Alhamisi , 8th Dec , 2016

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, amekuwa mchezaji wa sita kufikia nusu-karne idadi ya magoli katika chati za mabao za UEFA.

Karim Benzema

 

Benzema amefikisha magoli 50 kwenye Ligi ya Mabingwa katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Borussia Dortmund, iliyoisha kwa sare ya 2-2, Jumatano, akifunga katika dakika ya 28, baada ya kuunganisha krosi ya Daniel Carvajal na katika dakika ya 53 akafunga kwa kichwa.

Benzema anafikia rekodi ya Mfaransa mwenzake na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona Thierry Henry ambaye amefunga mabao 56.

Wengine waliofikia rekodi ya mabao mengi ya Uefa ni: Cristiano Ronaldo (95), Lionel Messi (93), Raul (71) na Ruud van Nistelrooy (56) pekee ndio waliofunga mabao mengi zaidi katika michuano hiyo ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya.