Alhamisi , 20th Apr , 2017

Chama cha kandanda la kulipwa nchini Uingereza (PFA) kimetangaza timu yake ya mwaka huku wachezaji wa Tottenham na Chelsea wakijaza nafasi nane kati ya nafasi 11.

Kante na Kane

Timu hiyo, ambayo ilipigiwa kura na vilabu vyote 92 vya Ligi ya Kandanda nchini Uingereza na vilabu vinane vya Ligi Kuu ya Wanawake, ina wachezaji watano ambao walikuwepo ndani ya timu ya msimu wa 2015-16.

Mlinda mlango wa Manchester United, David de Gea, kiungo wa Chelsea N'Golo Kante, na wachezaji watatu wa Spurs: Danny Rose, Dele Alli, na Harry Kane wote wamejumuishwa katika kikosi cha mwisho kwa msimu wa pili mfululizo. 

Hiki hapa kikosi chenyewe