Alhamisi , 29th Jan , 2015

Shirikisho la Soka nchini TFF limesema ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano nwa TFF, Boniface Wambura amesema, Waamuzi waliosimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo ambapo matokeo ya uchunguzi huo yatatangazwa na FIFA baada ya shughuli hiyo kukamilika.

Wambura amesema, wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA katika utendaji wao ambapo FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya.