Jumatatu , 29th Mei , 2017

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara (aliyefungiwa), ameendelea kukazia msimamo wake  kuwa klabu hiyo ndio mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu huu na mpaka sasa  kwa kudai wanasubiri majibu kutoka FIFA muda mfupi ujao. 

Haji Manara

Manara kupitia mtandao wake wa kijamii ameandika hayo kwa kuwataka mashabiki na wapenzi kuwa klabu hiyo ndio mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu huu.

"Simba ni bingwa wa kombe la Shirikisho, ni bingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu. Ndio ni bingwa wa nchi msimu huu, ni kusubiri tu wenye mpira wao FIFA,waturudishie points zetu tatu,zilizo wazi kwa kanuni zote,ili tutawazwe rasmi kuwa machampioni wa nchi hii" -Manara ameandika. 

Aidha Manara katika andiko lake amefunguka kuwa haiwezekani mchezaji mwenye kadi tatu za njano kushiriki mchezo huku akidai kwamba ni dhuluma kwa timu ya Simba pia ni  kinyume cha kanuniza mchezo huo.

"Yes, no way, mchezaji awe na kadi tatu za njano zilizothibitishwa, pasi na shaka yoyote na ripoti za waamuzi na makamisaa wa michezo husika na bodi ya ligi yenye jukumu halali la kikatiba la uendeshaji na usimamizi wa ligi, kisha eti kwa matakwa ya ajabu ya shirikisho na kamati yake isiyo na nguvu ya kisheria na kikanuni, iipoke points Simba,kwa sababu zozote zile, ni kanuni ambayo ipo wazi na ni dhulma isiyohitaji tochi kuiona, In Sha Allah , bingwa halali atatangazwa hivi karibuni"- Manara. 

Yes, ni ubingwa wa Jasho na damu,ni ubingwa uliotafutwa kwa nguvu zote halali na uliomwaga damu za wanasimba walioumia na kupoteza maisha yao,katika kuusaka ubingwa.