Jumanne , 5th Jul , 2022

Klabu ya Manchester United imekamilisha na kutangaza usajili wa beki wa kushoto Tyrell Malacia kutoka klabu ya Feyenoord ya Uholanzi kwa ada ya uhamisho iya pauni milioni 12 zaidi ya Bilioni 33 kwa pesa za kitanzania amesaini mkataba wa miaka 4.

Tyrell Malacia amejiunga na Manchester United kwa mkataba wa miaka 4

Taarifa ya Manchester united juu ya usajili wa beki huyu raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22 imesema.

''Manchester United tunapenda kuthibitisha kwamba Tyrell Malacia amejiunga na klabu yetu, na amesaini mkataba hadi Juni 2026 na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.’’ Imesema taarifa ya Manchester United

Malacia anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Manchester United chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Erik Ten Hag na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakacho safari siku ya Ijumaa kuelekea nchini Thailand na Australia ambako klabu hiyo itaweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya (Pre-season).

Kwa upande mwingine mchezaji mwenye amefurahishwa kujiunga na Manchester United.

''Ni hisia ya tofauti sana kujiunga na Manchester United. Huu ni ikurasa mpya kwangu, Ligi mpya na wachezaji wenza wapya na kocha mzuri anayetuongoza. Namjua kutokana na kucheza dhidi ya timu yake kwenye Eredivisie (Ligi kuu Uholanzi), sifa alizonazo na kile anachokitaka kutoka kwa wachezaji wake.’’Amesema Malacia

Malacia ameichezea Feyenoord jumla ya michezo 136 katika misimu 5 na amefunnga mabao 4, lakini pia ameichezea timu ya taifa ya Uholanzi jumla ya michezo 5 kati ya mwaka 2021 mpaka 2022.