Ijumaa , 4th Dec , 2020

Mashabiki wa mchezo wa soka nchini Uingereza wameruhusiwa kurejea viwanjani kushuhudia michezo mbali mbali huku wakisisitizwa kufuata utaratibu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa korona ambao bado upo nchini humo.

Mashabiki wa mpira wa miguu Uingereza wakionyesha ishara ya kufurahishwa na urejeo wao kushuhudia michezo viwanjani.

Mchezo wa Arsenal dhidi ya Rapid Vienne wa Europa uliochezwa usiku wa jana na kumalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa mabao 4-1 kwenye dimba la Emirates umeingia kwenye historia ya kuwa miongoni ya mchezo ya kwanza kushuhudiwa na mashabiki baada ya vizuizi kuisha Uingereza.

Mashabiki wapatao 2,000 wameushuhudia mchezo huo huku wengi wao wakielezwa kufurahishwa sana hatua hiyo.

Kwa Upande wa kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema hamasa ya mashabiki imechangia sana vijana wake kushinda mchezo huo.

Ikumbukwa kuwa serikali ya nchini Uingereza kupitia waziri mkuu wake Boris Johnson wametangaza kuendelea kuruhusu mashabiki kurejea kushuhudia michezo mingine kwenye EPL huku wakifuata tahadhari baada ya vilabu kupaza sauti kutaka mashabiki kurejea viwanjani ili waondokane na ukata.