Jumapili , 13th Aug , 2017

Timu ya TMT imechapwa na Mchenga BBall Stars kwa pointi 101-71 katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa fainali ya Sprite BBall Kings mchezo ambao umepigwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay huku ukishuhudiwa na wasanii na watu maarufu mbali mbali

Nahodha wa Mchenga BBall Stars, Mohamed Yusuph akimuwekea kizingiti nahodha wa TMT, Is-haka Masoud asiweze kuenda upande wa pili.

Kutokana na matokeo hayo, Mchenga BBall Stars imeweza kujiweka katika nafasi nzuri za mashindano haya ili kuweza kuwa mshindi wa jumla.

Pamoja na hayo, timu ya TMT ilionekana kuelemewa sana siku ya leo katika robo ya tatu ya mchezo jambo ambalo lilipelekea kuwapa wepesi wapinzani wao kuendelea kuongea pointi zaidi.

Kwa upande mwingine, TMT na Mchenga BBall Stars watakutana tena siku ya Jumatano ili kuweza kucheza 'game 2' ya fainali hizi.