Jumatatu , 18th Aug , 2014

Baada ya kuingiliana kwa ratiba ya kuutumia uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam kwa michuano ya Afrika ya mchezo wa Rollball na ile ya shule za sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki sasa Rollball yasalim amri nakuahirisha michuano yao

Wachezaji wa timu ya Tanzania [Tiger Rollball Club] wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Afrika.

Ambapo chama cha mchezo wa Rollball Tanzania TRBA kimesogeza mbele michuano ya mchezo huo kwa nchi za Afrika ambayo ilikuwa ianze August 26 mwaka huu jijini Dar es salaam

Rais wa TRBA Noel Kihunsi amesema sababu kubwa ya kusogeza mbele michuano hiyo ni kutokana na ratiba hasa tarehe ya kutumia uwanja wa ndani wa taifa kuingiliana na ratiba ya michezo ya shule za sekondari kwa nchi za Afrka Masharik FEASA

Kihunsi amesema wameamua kusogeza mbele michuano yao kwa kuzingatia hasa kuwa uwanja wa ndani wa taifa kwa wao watautumia kwa mchezo mmoja huku FEASA wakitumia uwanja huo kwa michezo takribani 4 hivyo ni bora kuahirisha shindano la mchezo mmoja kuliko kuahirisha shindano la michezo mingi

Aidha Kihunsi amesema wamejadiliana na TAMISEMI kuhusu suala hilo na kukubaliana kusogeza mbele na wametuma taarifa juu ya suala hilo kwa chama cha Rollball Afrika ili watoe baraka zao kwa ajili ya tarehe mpya ya mashindano hayo ambayo wao wamependekeza yafanyike tena mwezi wa kumi.