Jumatatu , 22nd Mei , 2017

Uongozi wa Kagera Sugar umewashukuru mashabiki wa timu yao kwa kuwaonesha uzalendo wa hali ya juu katika kipindi chote walichopitia katika michuano hadi kuibuka washindi  wa tatu ligi kuu Tanzania Bara.

Kikosi cha Kagera Sugar mara baada ya kukabidhiwa medali za mshindi wa tatu

Kupitia ukurasa wao instagram, Kagera Sugar imesema kuwa bila ya mashabiki zao, wasingeweza kupata mafanikio waliyoyapata katika msimu huu katika soka.

"Special thanks' za dhati ziende kwa mashabiki wetu wakiongozwa na kikundi chetu cha uhamisishaji na ushangiliaji mmetoa sana mchango mkubwa kufanikisha mafanikio yetu msimu huu... Mmekuwa bega kwa bega na sisi kama timu kwa vipindi vyote vigumu na vile vya furaha tuliposhinda tulishangilia pamoja na tuliposhindwa tulihuzunika pamoja.....Tunzo yenu ya mchezaji bora wa mechi katika kila mchezo iliongeza na kutia chachu kwa kila mchezaji ndani ya kikosi ".Ilisema taarifa hiyo kutoka Kagera

Katika hatua nyingine, klabu hiyo iliwapongeza wachezaji wake Juma Kaseja kwa kuchaguliwa kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya kipa bora pamoja na Mbaraka Yusuph kuteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika ligi hiyo.