Ijumaa , 30th Jan , 2015

Pambano la Ubingwa wa Afrika wa UBO linatarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha Issa na Nampepeche akipanda Ulingoni na Nassib Ramadhani katika Pambano hilo la Roundi 10.

Kwa upande wake Nassib Ramadhan amesema anatarajia kufanya vizuri katika pambano hilo kutokana na mazoezi aliyonayo mpaka hivi sasa ambapo ameshapigana mapambano 20 na kushinda 14.

Kwa upande wa Issa Nampepeche amesema amejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo la kuanza mwaka kwa upande wake na ana amini pambano hilo halitompa shida ambapo mpaka sasa ana mapambano 22 na ameshinda 19 na kupoteza mapambano mawili.