Jumatano , 20th Oct , 2021

Klabu ya Newcastle United imeachana na kocha wao Steve Bruce baada ya wamiliki wapya wa klabu hiyo kuhitaji mabadiliko ya kocha baada ya kudumu na timu kwa zaidi ya miaka miwili.

Picha ya Kocha Steve Bruce

Hivi sasa wapo kwenye mpango wa kumpata mrithi wake  kabla ya mchezo wao dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki hii huku Paulo Fonseca kocha wa zamani wa Roma, Lucien Favre na Eddie Howe wanatajwa kuchukuwa nafasi yake pale St. James' Park.