Mwanzoni mwaka jana Azam FC ilithibitisha kuachana na Kiungo huyo wa zamani wa klabu za Simba SC na Young Africans zote za Dar es salaam, na kumtakia kila la kheri katika makazi yake mapya kisoka.
Ajibu amesema kwa sasa anaendelea kujiandaa vizuri huku akimuomba Mwenyezi Mungu amjaalie afya njema, ili kufanikisha mpango aliojiwekea, baada ya kuondoka Azam FC.
“Namuomba Mungu anipe afya njema nataka kwenda kuonyesha mfano, siyo kama nilishindwa kucheza Azam FC kwa ajili ubora, binafsi sipendi kuongea bali nitakwenda kuonyesha vitendo,”amesema Ajibu
Kiungo huyo ambae mwaka jana ametambulishwa katika klabu ya Singida Bigstar kwa mkabata wa miaka miwili vile Ajibu atakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa kwenye kikosi hicho baada ya beki wa kushoto, Nickson Kibabage aliyesajiliwa kutokea Mtibwa Sugar