Alhamisi , 8th Dec , 2016

Uongozi wa Klabu ya Simba umewataka wanachama kuhudhuria mkutano unaotarajiwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu ili kila mwenye wazo aweze kuchangia kwa maendeleo ya klabu.

Geoffrey Nyange 'Kaburu'

 

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geoffrey Nyange Kaburu amesema mwenye mamlaka ya kuitisha Mkutano Mkuu wowote kulingana na katiba ni Rais akishirikiana na Kamati ya Utendaji na hakuna mtu yeyote anayehusika kusitisha mkutano..

Kaburu amesema, ili uwe mwanachama wa Simba ni lazima uwe mtiifu wa Simba kwa kufuata katiba na siyo kuvunja katiba, hivyo mkutano upo palepale na wanachama wanatakiwa kuitikia wito kwani mkutano ndiyo sehemu pekee ya kuonana na uongozi na hata kama hawahitaji mabadiliko wanatakiwa kufika ili kutoa hoja zao ambazo zitasikilizwa ili kuweza kufanya maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya klabu.

Kaburu amesema, kwa wale wanaopinga mabadiliko wanatakiwa kusoma upya katiba na kama wana lolote la kuongea wafike kwenye mkutano ili kuweza kuchangia kwa manufaa ya klabu.