Jumatatu , 2nd Jan , 2023

Kikosi cha Yanga kikiongozwa na kocha Cerdic Kaze kimesafari leo majira ya saa 10:00 jioni ya leo kuelekea Zanzibar, kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo yameanza rasmi januari 1, 2023

Katika msafara wa leo wa kikosi cha Yanga ulioelekea Zanzibar, Mayele hakuwa kwenye kikosi hicho.

Nyota wengine ni Aziz Ki, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Yannick Bangala ambapo wote hawa wamepewa mapumziko.

Kwa mujibu wa meneja wa kikosi cha Yanga, Walter Harrison amesema kuwa sababu ya kuwatumia vijana kwenye Kombe la Mapinduzi Cup ni kuwapa uzoefu pamoja na uwezo ambao wanao.

“Wachezaji wote wana uwezo na tumechanganya wachezaji wa timu kubwa pamoja na ile ya vijana lengo ni kuona wanapata uzoefu na kuleta ushindani,”amesema Meneja wa Yanga Walter Harrison

Ni Januari 4 Yanga itakuwa na mchezo wake wa kwanza katika Mapinduzi dhidi ya KMKM.