Saturday , 23rd Dec , 2023

East Africa TV na East Africa Radio kupitia kampeni ya Namthamini tumekabidhi taulo za kike pakiti 2632 siku ya leo kwa wahanga wa Katesh katika wilaya ya Hanang, Manyara.

Balozi wa kampeni ya Namthamini, Justine Kessy akikabidhi taulo za kike kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja.

Balozi wa kampeni ya Namthamini Justine Kessy amekabidhi taulo za kike zipatazo pisi 2632 kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja ambazo zitaweza kuwasaidia wanawake na mabinti zaidi ya 200 kwa kipindi cha mwaka mzima.