Alhamisi , 22nd Apr , 2021

Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) imesema kufuatia uwekezaji uliofanywa katika mradi wa Mlimani City unaosimamiwa na mwekezaji Mlimani Holdings Limited kusaidia katika kupatikana kwa ajira zaidi ya elfu mbili na kodi za serikali inatarajia kufungua miradi kama hiyo Dodoma na Arusha.

Muonekano wa Jengo la Ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kauli hiyo imetolewa hii leo mara baada ya ujumbe wa wataalamu kutoka Kutoka Kituo Cha Uwekezaji TIC waliotembelea kwa mwekezaji huyo ili kutazama changamoto alizopitia mara baada ya Covid-19 na changamoto zingine ili kuzipatia ufumbuzi.

Amesema serikali inaendeleza kuweka mazingira kwa kasi ikiwataka wawekezaji wa ndani na nje kuzidi kujitokeza kwa kuwa nchi ya Tanzania ina mazingira tulivu ya kisiasa.

"Tunatarajia Uwekezaji kama huu kufanywa katika Jiji la Dodoma utasaidia ajira na kodi kwa Serikali  sisi kama serikali TIC tunazidi kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje", amesema Bevin Ngize.

Kwa upande wa mwekezaji huyo amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwatambua wawekezaji kuwasaidia akibainisha wako tayari kuendesha miradi hiyo popote hapa nchini kwa kibali cha serikali.

"Mradi huu tangu mwaka 2004 umeanza Hapa kuna biashara za aina zote kumbi za mikutano na mazingira haya ambayo serikali yametupa nafuu sisi kama wawekezaji", amesema Mroso.