Kampeni ya kibiasharazaidi yaleta chachu ICEALION

Jumatatu , 27th Jul , 2020

Mkuu wa Operesheni wa Kampuni ya Bima ya ICEA LION, Jared Awando, amesema kampeni ya Kibiashara Zaidi iliyoendeshwa na kampuni ya EATV Limited kupitia televisheni, radio na mitandao yake kijamii imeleta mwamko chanya kwa watumiaji na wawekezaji katika soko la bima nchini.

Akizungumza na EATV SAA 1 katika hafla ya kuwapongeza wabia ambao ni wakala wa bima kupitia kampuni hiyo Bw. Awando amesema katika kipindi cha miezi sita wakala wameongezeka kutoka 12 wa awali hadi kufikia 45 ikiwa ni sawa na asilimia 93 hivyo kuwafanya kuwa imara zaidi katika utoaji wa huduma ya bima nchini.

Kwa upande wao wakala wa bima wabia wa ICEA LION wamesema kuwa hamasa hiyo waliipata baada ya kufuatilia EATV na East Africa Radio kupitia kampeni yake Kibiashara Zaidi na kuongeza kuwa hadi wametumia fursa hiyo kuongeza mapato pamoja na kukuza soko la ajira nchini.

Kampeni ya Kibiashara Zaidi ilikuwa na lengo la kuhamasisha na kuchochea shughuli za kibiashara nchini katika kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia biashara mbalimbali, ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dk. John Maagufuli za kuwahamasisha Watanzania kujikwamua kiuchumi kwa kushiriki katika biashara.