Jumanne , 24th Mei , 2022

Licha ya Dunia kukumbwa na ugonjwa wa UVIKO-19 ambao uliathiri baadhi ya shughuli za uchumi katika maeneo mbalimbali, lakini lipo kundi jingine ambalo lilioona fursa na kuitumia vizuri kuongeza kipato.

Idadi ya matrilionea duniani imefikia 2,668

Kila baada ya masaa 30 mtu mmoja anaingia katika orodha ya matrilionea duniani, kuanzia mwaka 2020 mpaka kufikia mwezi huu wameongezeka matrilionea 573 duniani kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Oxfam.

Matrilionea wengi wametoka katika biashara ya chakula, nishati, na sekta ya dawa. matrilionea 62 wametoka katika biashara ya chakula, matrilionea 40 wametoka katika biashara ya dawa, huku wafanyabiashara wa mafuta wametajwa wanaingiza faida ya dola 2,600 kila baada ya sekunde moja.