Jumatano , 19th Aug , 2020

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashantu Kijaji, amezitaka Taasisi za Kifedha nchini kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukuza mitaji yao.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Ashantu Kijaji.

Dkt Kijaji ametoa kauli hiyo leo Agosti 19, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Makao Makuu ya Benki ya NCBA pamoja na ofisi zake

Mbali na hayo Dkt Kijaji amezishauri Taasisi hizo pia kupeleka huduma zake mpaka maeneo ya vijijini kutokana na wananchi wengi wa maeneo hayo kukosa huduma za Kibenki.

Kwa upande wake Meneja Msimamizi wa Taasisi za Fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania, Nassor Omari ameeleza mipango ya Benki Kuu kwa taasisi hizo za kifedha huku Mkurugenzi Mkuu wa NCBA Benki Magreth Karume, akiwataka wananchi kutegemea huduma bora za kifedha kutoka benki hiyo.