Jumatatu , 10th Aug , 2020

Ongezeko la uwazi katika uwekezaji, usalama na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji nchini umetajwa kuwa chachu ya kuongezeka kwa wawekezaji nchini.

Ongezeko la uwazi katika uwekezaji, usalama na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji nchini umetajwa kuwa chachu ya kuongezeka kwa wawekezaji nchini.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu Soko la Hisa la Dar es Salaam DSE Moremi Marwa ambapo amesema licha ya nchi mbalimbali kutetereka katika uwekezaji haswa wa hisa kutokana na Covid-19 bado Tanzania wawekezaji wa ndani na nje wameendelea kuamini mazingira ya uwekezaji.

"Sio mataifa makubwa tu yakiwemo Marekani,Japan na mengine ambayo yameathirika na suala la Covid 19 Kenya imetajwa kushuka zaidi na hali hii hutokea wakati wote kukiwa na majanga ila baada ya msimu ila wengi kufanya maamuzi kwa kitu ambacho hakina athari sana"

Moremi ameshauri wawekezaji kutumia msimu huu ambao masoko mengi ya dhamana na mitaji yameonekana kushuka haswa kwenye hisa kwani bado ni uwekezaji ambao unafaida wakati soko litakapoimarika.

"Wawekezaji wengi wamewekeza katika hatifungani za serikali ambayo mara nyingi yametajwa kuwa na uhakika wa kupata fedha zao inafanyika katika mataifa mbalimbali maana hiyo ni mbinu ya kibiashara"