Jumatatu , 12th Dec , 2022

Nchi 15 za bara la Africa zimekutana nchini Tanzania na kufanya kongamano lililolenga kupeleka ujumbe katika nchi hizo Kwa ajili ya kupata uelewa wa mkataba wa kimataifa ambao nchi hizo zitaufuata na kuweka sheria na kanuni juu ya namna bora ya kudhibiti uharibifu baharini

Akizungumza katika kongamano Hilo litakalodumu Kwa muda wa siku tatu kuanzia Leo Naibu Katibu Mkuu wizara ya ujenzi na uchukuzi Dkt Ally Possi amesema Mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la kimataifa la IMO na Tanzania kuwa mwenyeji unaumuhimu Kwa nchi ya Tanzania kwani utaiwezesha nchi kuzingatia makubaliano ya kiitifaki ya sheria ya kimataifa ya kuhakikisha vyombo vya usafiri wa Maji havichafui bahari, maziwa na mito Kwa sababu ya utunzaji wa mazingira katika maji

Amesema Kwa Sasa Hali ya utunzaji wa mazingira katika maji ni nzuri na tahadhari zinaendelea kuchukuliwa Kwa ajili ya kulinda viumbe waishio baharini, ziwani na kwenye miyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la uwakala wa meli Tanzania-TASAC, Kaimu Abdi Mkekenge ameeleza kwamba Mkutano huo utaiwezesha nchi kufanya vizuri zaidi katika kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa bluu.