Jumatatu , 10th Aug , 2020

Mratibu wa programu na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Nyakaho Mahemba amesema serikali imelenga kuwawezesha wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa katika kutatua changamoto za mitaji nchini.

Bi. Nyakaho ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio na kuhimiza kuwataka raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na zaidi kuchangamkia fursa ya kupatiwa mitaji wakiwa katika vikundi ama mtu mmoja mmoja ili kuwawezesha katika shughuli za uzalishaji.

Aidha, Bi. Nyakaho amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo SIDO na taasisi ya elimu na vyuo vya ufundi VETA imeweka makubaliano ya utoaji wa elimu ya namna ya kutambua fursa za uwekezaji katika jamii.

Ikumbukwe kuwa mpango huu ulizinduliwa mjini Dodoma tarehe 10 Julai mwaka huu na waziri wa nchi, bunge, sera, mipango na watu wenye ulemavu Bi Jenista Mhagama na kupewa jina la Sanvin Viwanda Scheme ukiwa ni mpango jumuishi wa kuendeleza viwanda vidogo na vya kati nchini