Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

SBL yaja na kampeni kuinua mfumo wa biashara

Jumatano , 19th Jul , 2023

Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua kampeni yake ya kitaifa 'Jibambe Kibabe' inayolenga kuchochea uwezeshaji kiuchumi katika mfumo wake mzima wa biashara.

Irene Mutiganzi, Mkuu wa Masoko ya Vinywaji Vikali, Serengeti Breweries Limted

Kampeni hiyo itatoa motisha, marejesho ya fedha, na punguzo kwa washirika wake wa biashara wanaponunua bia na vileo vya SBL. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, 2023 Mkuu wa idara ya Vileo  kutoka SBL, Irene Mutiganzi, amesema, washindi wa kampeni ya 'Jibambe Kibabe' kutoka mtandao wa biashara wa SBL ni pamoja na wauzaji wakubwa, wauzaji jumla, wasambazaji na maduka ya rejareja.

"Kampeni ya 'Jibambe Kibabe' imeanzishwa kwa  lengo la kuwawezesha washirika wa kibiashara wa SBL, haswa katika mazingira ya uchumi ya sasa ambapo biashara zinakaribia kupona kutokana na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi katika miaka kadhaa iliyopita." Amesema Mutiganzi.

Akifafanua kuhusu muundo wa kampeni hiyo, Mutiganzi amesisitiza kuwa kampeni hiyo inawapatia wateja wanaofanya vizuri punguzo na marejesho ya fedha, na pia kuwapa fursa ya kupata soko kutokana na athari inayotarajiwa ya kampeni hiyo inayosukuma ununuzi zaidi. 

Aidha, kampeni hiyo pia inajumuisha kipengele kinachowazawadia wafanyakazi wa baa kwa kila chupa wanayouza kwa kufikia malengo yao.

Wengine wanaonufaika na 'Jibambe Kibabe' ni watumiaji katika kiwango cha baa ambapo kampeni hiyo imeandaa ofa za kubebea (bucket deals) zilizo tengenezwa maalum kwa watumiaji kufurahia na kushiriki na marafiki kwa bei iliyopunguzwa, hatimaye kutoa akiba kwa wote.

Naye, Nicholas Chonya, Meneja Mauzo wa Serengeti Kanda ya Dar es Salaam amesema kampeni hiyo itahusisha vinywaji vyetu vyote, kwa maana ya bia na baadhi ya pombe kali zinazotengenezwa na kampuni ya bia ya Serengeti.  

"Nitoe wito na msisitizo kwa washirika wetu wa kibiashara, kuanzia wasambazaji mpaka mlaji wa mwisho, kushiriki kwa wingi," alisema Chonya na kuongeza.

"Kwa mfano kupitia kampeni hii, wauzaji wa baa wanaofikia asilimia 50  ya malengo yao ya mauzo watajipatia kiasi cha fedha kuanzia shilingi 100 kwa chupa moja ya bia, hadi Sh. 1,000 kwa chupa moja ya pombe kali."  

Kwa upande wake mwakilishi wa wasambazi wa vinywaji vya Serengeti, Jonas Sindabaha, alisema anawapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuandaa kampeni hii ya 'Jibambe Kibabe' ambayo imelenga kuwanufaisha wanaofanya nao biashara kwa ukaribu. 

"Hii inatudhihirishia kuwa Serengeti ni washirika wetu wa kibiashara wa kweli, wanaojali maslahi yetu. Hivyo niwapongeze kwa hatua hii," alisema Sindabaha.

Mwisho

HABARI ZAIDI

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ