Jumanne , 21st Jun , 2022

Kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kutoa maagizo matano kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa ikiwemo kudhibiti baadhi ya wafanyabiashara kutorejea kwenye maeneo yaliyokatazwa EATV imepita katika mitaa kuona uhalisia ulivyo.

EATV imeshughudia wafanyabiashara wakiwa katika maeneo yao ya biashara na mengi yakiwa ni maeneo yanayoruhusiwa kufanya biashara ambapo baadhi ya wafanyabiashata wameeleza hali ilivyo

"Sisi hapa tangu zoezi lianze la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo sisi tulipewa namba maalum sasa hii ni rai kwa wengine sio watoke huko waje tuu kupanga bila kuwa na utaratibu watabebewa biashara zao" alisema Japhet Mafuru Mfanyabiashara Machinga Complex

EATV imefika kwenye ofisi ya mweyekiti wa Mtaa wa Kigogo kati kujua hali ikoje katika mtaa huo kuhusu mpangilio wa Wafanya biashara.

"Mimi kwenye mtaa wangu wafanyabiashara wote tuliowapanga bado hawajarudi kwenye maeneo yaliyokatazwa nitoe wito kwa viongozi wenzangu kusimamia maagizo" alisema Rashid Luoga Mwenyeti wa Mtaa wa Kigogo kati.

Hata ivyo waswahili wanasema sheria ni msumeno ambapo watalaamu wa sheria wanasema kutumia eneo kwa kujinufaisha ambalo si lako kihalali ni makosa Kwa mujibu wa sheria hivyo kuwataka wafanya biashara wanaolazimisha kurejea kwenye maeneo yaliyokatazwa kuacha mara moja.