Jumatano , 5th Apr , 2023

Wakazi wa kata ya kinzudi Manyema Manispaa ya Ubungo wamesema wanalazimika kulipa hadi shilingi elfu tatu kupanda boda na bajaji kwenda zilipo daladala kutokana na uharibufu wa miundo mbinu ya barabara uliopo wakibainisha kuwa hali inakuwa mbaya zaidi kipindi cha mvua kama hiki.

Kufuatia mwendelezo wa mvua zinazoendelea kunyesha EATV imefika katika kata hiyo ambayo ukitokea Africana hadi mwisho wa lami inapakanisha manispaa ya kinondoni na Ubungo,wakazi hao wameeleza namna ambavyo usafiri ni tatizo kubwa kwa wamama wajawazito na watoto ambao hawawezi kujipambania.

Uhalisia wa barabara ulivyo unawafanya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wameeleza namna ambavyo wengine hulazimika kuacha kutumia vyombo vyao kutokana na ubovu wa barabara.

Wakazi wa kinzudi wamelazimika kufikisha kilio chao cha ubovu wa barabara kwa serikali kutokana na madhila ya muda mrefu wanayopitia kwa vipindi vyote vya mwaka.