Jumatano , 28th Apr , 2021

Mtendaji mkuu wa Soko la hisa  la Dar es salaam, Moremi Marwa amesema Wawekezaji mmoja mmoja katika Soko la hisa wameonekana kufanya uwekezaji mkubwa na hasa katika hati fungani za serikali kwa kuwa ni imara na zenye uhakika.

Moremi Marwa - Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE

Akitoa Taarifa ya wiki iliyoishia terehe 23 April 2021, amesema kwa sasa serikali inauza hati fungani kwa wingi ili kuelekeza fedha hizo katika sehemu ya bajeti yake pamoja na miradi ya kimkakati.

"Watu wengi zaidi wanaupenda hizi hati fungani za serikali kwakuwa kwanza zinauhakika na hususani zile za muda mrefu nyingi zina faida kubwa", amesema Moremi Marwa - Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE.

Sambamba na hilo, taarifa yake imeeleza kuwa wawekezaji wa ndani walitawala katika miamala ya  manunuzi ya hisa huku asilimia 96 ya mauzo ya hisa ikichangangiwa na wawekezaji kutoka nje.