Jumatatu , 3rd Oct , 2022

Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss amelazimika Jumatatu kubadilisha mipango ya kupunguza kiwango cha juu zaidi cha ushuru wa mapato ambayo yaliibua uhasama katika chama chake na kuchochea msukosuko katika soko la fedha.

Liz Truss, Waziri Mkuu wa Uingereza

Truss, na waziri wake wa fedha Kwasi Kwarteng, walitangaza "mpango mpya wa ukuzaji uchumi" mnamo Septemba 23 ambao ungepunguza ushuru na udhibiti, kwa kuongeza ukopaji mkubwa wa serikali ili kuondoa mdororo wa uchumi uliokwama kwa miaka mingi.

Saa chache tu baada ya Truss kwenda kwenye runinga ya BBC kutetea sera hiyo, Kwarteng alitoa taarifa akisema anakubali imekuwa kikwazo kutoka kwa juhudi pana za kusaidia kaya wakati wa baridi kali. Kutokana na hilo, ametangaza kwamba hawaendelei na kufuta kiwango cha kodi cha asilimia 45. 

"Kutokana na hilo, natangaza kwamba hatuendelei na kufuta kiwango cha kodi cha asilimia 45. Tumewaapata, na tumewasikiliza," alisema katika taarifa hiyo.