Hong Kong imekabiliwa na moto mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa ambao umegharimu maisha ya watu 55, huku watu 279 wakiwa hawajulikani walipo, wakati tahadhari juu ya hali kuwa mbaya zaidi ikiendelea kutolewa.
Moto huo ulizuka mwendo wa saa sita mchana jana Novemba 26 kwenye jumba la makazi la ghorofa 31 huko Tai Po, linalojumuisha zaidi ya vyumba 1,900 na makazi ya karibu wakazi 4,800.
Polisi wamewakamata wanaume watatu -mameneja wawili na mhandisi mshauri kutoka kampuni ya ujenzi inayoaminika kufunga vifaa vya ukarabati vinavyoweza kuwaka moto kwa tuhuma za mauaji hayo.
Wakazi wa majengo mawili ya jirani pia walihamishwa, idadi ya watu wanaofikia 900 sasa wanajihifadhi katika vituo vya muda. Zaidi ya magari 140 ya zima moto na zaidi ya wafanyakazi 800 wa dharura wametumwa kukabiliana na moto huo.



