Balozi wa pamba Tanzania Aggrey Mwanri
Balozi huyo ameitoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuwataka kuzunguka Kijiji kwa Kijiji kutoa elimu kwa wakulima ili wajue zao la pamba ni zao lenye soko la uhakika.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru, amewaahidi watumishi wa wilaya hiyo kuwa mbabe kwa yeyote atakayeshindwa kuwajibika shambani kwa kumpa elimu mkulima na kusubiri kuwasumbua magetini kwa kuwatoza tozo.






