
Ilipotangazwa mwaka jana, mataifa ya magharibi na wanaharakati walitumaini kuwa inaweza kutoa mfano wa kumaliza utegemezi wa makaa ya mawe.
Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya zimeahidi makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 8.5 ambayo yanajumuisha mipango ya kuwasaidia wafanyakazi wa mafuta kuhamia kwenye viwanda vya kijani.
Rais huyo wa Afrika kusini amesema kwamba walipoangalia kwa ukaribu zaidi tukribaini asilimia 2.7 tu ndiyo ilikuwa fedha za ruzuku.
Viwango vingine ni mikopo Afrika Kusini tayari inabeba mzigo mkubwa wa mkopo, ambapo amesema wanahitaji ufadhili zaidi wa ruzuku.