Raia wa China Sheng Beng Lin aliyehukumiwa miaka mitatu, ambapo amelipa faini na kubaki huru.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Theopista Sivoke, baada ya raia huyo wa China anayefahamika kwa jina la Sheng Bing Lin, kukiri kutenda kosa hilo kwa kumshawishi Afisa Mtendaji ampe rushwa ili amrudishie mashine yake.
Awali akitoa taarifa ya kukamatwa kwa raia huyo wa kigeni Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Daudi Ndyamukama, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Ambapo mara baada ya hukumu hiyo kutolewa, Sheng Bing Lin alifanikiwa kulipa faini hiyo na kubaki huru.

