 
Kwa Mujibu wa Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe miongoni mwa ajenda ambazo zitajadiliwa leo ni pamoja kuzuia wabunge kufanya Kazi zao za ubunge kwa sababu ya kutaka wananchi waendelee kuona Bunge live.
Tishio la nchi kwenda kwenye utawala usioheshimu sheria kwa kuminya uhuru wa Bunge, Mahakama na CAG, Pia maamuzi ya hovyo ya serikali kuhusu wanafunzi wa UDOM.
Aidha suala la bajeti ya kwanza ya Rais Magufuli litajadiliwa katika mkutano huo ambao ni wa kwanza kabla ya safari ya kwenda katika maeneo mengine nchini ambapo UKAWA na wenyewe wametangaza kuwa na mikutano kama hiyo ya kuelimisha umma pamoja na mambo yanayohusu Bunge, serikali na wananchi.

 
 

 
 
 
 
 
