Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Alichokisema Mtatiro baada ya kuteuliwa na Rais

Jumapili , 14th Jul , 2019

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama Cha wananchi (CUF) Julius Mtatiro, ambaye alitangaza kuhamia CCM kutokana na chama chake cha CUF kukabiliwa na migogoro ya kiuongozi.

Uteuzi wa Julius Mtatiro umetangazwa na Rais wa Magufuli leo asubuhi ya Julai 14, 2019, akiwa wilayani Chato kwa mapumziko binafsi, ambapo uteuzi huo unatarajia kuanza mara moja kuanzia leo Jumapili.

Kabla ya Mtatito kushika nafasi hiyo, awali ilikuwa ikishikiliwa na Juma Homera ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Akizungumzia uteuzi huo, Julius Mtatiro amesema kuwa, "nimezipokea taarifa nikiwa safarini tena, tena nimezipokea kwa mshtuko sana, kwa sababu sikutarajia kwamba naweza kuteuliwa na Rais, unajua ukiteuliwa halafu hukuwa unatarajia unapata mshtuko sana."

"Ila ukimaliza kupokea kwa mshtuko hizo taarifa inabidi ukubaliane nazo tu, kwa sababu ni kazi ya umma na hakuna budi kuitumikia", amesema Mtatiro.

Agosti 11, 2018 kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, Mtatiro alitangaza kujiondoa Chama Cha Wananchi CUF, kwa kile alichokieleza alikosa nafasi nzuri ya kuwatumikia Watanzania na kumaliza matatizo yao.

Sikiliza mahojiano kamili na Mtatiro, Bonyeza hapo chini

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya